Tone

Tone
Home » » WATENDAJI TENGENI MUDA WA KUWAHUDUMIA WANANCHI-MAJALIWA

WATENDAJI TENGENI MUDA WA KUWAHUDUMIA WANANCHI-MAJALIWA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wa Buchosa wakati alipoingia kwenye uwanja wa michezo wa Nyehunge wilayani Sengerema kuhutubia mkutano wa hadhara Februari 15, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa mmiliki wa kiwanda kidogo cha Dotto Posho Mill, Bw. Alexander Dotto (kushoto) kuhusu unga na Mchele unaozalishwa na kiwanda hicho kilichopo eneo la Bukara, Sengerema Februari 15, 2018. Kulia ni Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Miongella.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi wa Sengerema baada ya kuweka jiwe la msingi la kiwanda kidogo cha kusaga nafaka na kukoboa mpunga cha Dotto Posho Mill kilichopo eneo la Bukara, Sengerema Februari 15, 2018.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka watendaji na wakuu wa idara mbalimbali kuhakikisha wanatenga muda na kwenda vijijini kuwahudumia wananchi.Amesema wananchi hususani waishio maeneo ya vijijini wanachangamoto mbalimbali ambazo zinatakiwa kupatiwa ufumbuzi na watendaji hao.

Aliyasema hayo jana (Alhamisi, Februari 15, 2018) alipozungumza kwa nyakati tofauti na watumishi na wananchi katika kata ya Nyehunge na Ibisabageni wilayani Sengerema akiwa katika ziara ya mkoa wa Mwanza.
Alisema Serikali imedhamiria kwa dhati kuwatumikia kwa lengo la kuwaondolea kero mbalimbali zinazowakabili, hivyo hakuna sababu ya watendaji kukaa maofisini.“Watumishi wanawajibu wa kuwafuata wananchi katika maeneo yao hasa vijijini kwa sababu si kila mwananchi anauwezo wa kufuata huduma katika ofisi zenu na atakayeshindwa kufanya hivyo hatutomvumilia.”
Waziri Mkuu aliongeza kuwa Serikali inawawezesha watumishi wake kwa kuwapatia vitendea kazi kama usafiri ili waweze kuwahudumia wananchi ipasavyo.Alisema kwa sababu ya kutotekeleza wajibu wao ipasavyo kumekuwa na kero na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi na hivyo kusababisha wananchi kuwasilisha kero na malalamiko hayo wakati wa ziara za viongozi wakuu.
Katika hatua nyingine Waziri Mkuu aliwataka wananchi wanaofanya kazi katika kiwanda cha kuongeza thamani ya mazao ya nafaka cha Doto Alex Posho Meel kuwa waaminifu.Waziri Mkuu alisema wafanyakazi hao wanatakiwa wawe waaminifu na wafanye kazi kwa bidii ili kukiwezesha kiwanda hicho kuendelea na uzalishaji.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
ALHAMISI, FEBRUARI 16, 201

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mwanza Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa