Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongela (wa pili kulia, akikagua banda la Benki Kuu, kwenye Maonesho ya Nanenane yanayofanyika kwenye uwanja wa Nyamuhongolo Jijini Mwanza, kwa mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Na BMG
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John
Mongela, ameiagiza Mamlaka ya Usimamizi wa Biashara Tan-trade kukamilisha ramani ya viwanja vya Nyamuhongolo vinavyotumika kwa maonesho ya Wakulima na Wafugaji Nanenane ili kuanza ujenzi wa majengo ya kudumu kwenye viwanja hivyo.
Akifungua rasmi jana maonesho ya Nanenane yanayohusisha mikoa ya Kanda
ya ziwa, Mongela, alisema kukamilika kwa ramani hiyo kutaharakisha kuanza kwa ujenzi wa mabanda ya kudumu kwenye viwanja hivyo ili kuwezesha kuendelea kwa shughuli mbalimbali hata maonesho yatakapomalizika.
Alisema mkoa wa Mwanza kwa kushirikiana na mikoa mingine ya kanda ya ziwa, umejipanga kuandaa maonesho ya Nanenane kitaifa ndani ya miaka miwili ijayo, hivyo ujenzi wa mabanda hayo utachangia kuongeza hamasha ya mikoa hiyo kuwa mwenyeji.
Aidha mkuu huyo wa mkoa wa Mwanza ameungana na mwenzake wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack, kuwahamasisha wakulima wa mikoa hiyo kufufua kilimo
cha pamba ambacho amesema kitachangia kufufua viwanda mbalimbali na kuongeza fursa za ajira hasa kwa vijana na hivyo kukuza pato
la familia na taifa kwa ujumla.
Kwa upande wao baadhi ya washiriki wa maonesho hayo zikiwemo taasisi za serikali na wajasirimali, wamesema kumekuwa na mwamko mkubwa wa wananchi kutembelea maonyesho hayo tofauti na maonesho ya miaka iliyopita.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya maonesho hayo, Damian Chang’a, amesema maonesho ya mwaka huu yanashirikisha jumla ya Halmashauri 18 kutoka mikoa ya Mwanza, Geita, Shinyangana na Mara huku mikoa ya Simiyu na Kagera ikishindwa kushiriki.
Itakumbukwa kwamba, alieyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Evarist Ndikilo, ambaye sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, nae aliwahi kutoa ahadi kama aliyoitoa Mongela, katika Maonesho ya Nanenane miaka iliyopita.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongela, akisaini kitabu cha wageni kwenye banda la Benki kuu, kwenye maoneshp ya Nanenane Jijini Mwanza.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongela (kushoto), akifuatilia jambo kwenye maonesho ya Nanenane Jijini Mwanza.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack (kushoto) akiteta jambo na Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella (kulia).
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye Maonesho ya Nanenane Kanda ya Ziwa.
Burudani ya asili kutoka kikundi cha ngoma za asili Bujora
Mchezo wa nyoka kutoka Bujora
Wapiga picha wakifuatilia wacheza ngoma kutoka Bujora
Taasisi ya Kuzuia na Kutokomeza Ukatili wa Watoto Majumbani, Foundation Karibu Tanzania pia inatoa elimu kwenye Maonesho ya Nanenane Jijini Mwanza.
0 comments:
Post a Comment