Home » » PSPF YATOA MSAADA WA VIFAA VYA KUSOMEA KWA WANAFUNZI WAISHIO KATIKA MAZINGIRA MAGUMU MKOANI MWANZA

PSPF YATOA MSAADA WA VIFAA VYA KUSOMEA KWA WANAFUNZI WAISHIO KATIKA MAZINGIRA MAGUMU MKOANI MWANZA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Wanafunzi wa shule ya Msingi Igaka iliyopo Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza wakifurahia msaada uliotolewa na PSPF kwa wanafunzi waishio katika mazingira magumu shuleni hapo.
 Afisa Uhusiano wa PSPF, Bibi Coleta Mnyamani ,akiongea na kamati ya shule ya Msingi Igaka (ambao hawapo pichani) pamoja na wanafunzi kuhusiana na lengo la Mfuko wa Pensheni wa PSPF kusaidia jamii hasa kwenye nyanja ya elimu nchini.
Wanafunzi waishio katika mazingira magumu wa shule ya Msingi Igaka iliyopo Wilayani Sengerema wakipokea msaada wa mabegi yenye vifaa vya kusomea kutoka Mfuko wa Pensheni wa PSPF.
Wanafunzi waishio katika mazingira magumu wa shule ya Msingi Igaka iliyopo Wilayani Sengerema wakipokea msaada wa mabegi yenye vifaa vya kusomea kutoka Mfuko wa Pensheni wa PSPF.
Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Igaka, Bw. Jumanne Masumbuko, akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wanafunzi wenzake kwa masaada wa mabegi ya shule yenye vifaa vya kusomea kutoka Mfuko wa Pensheni wa PSPF.
Afisa Mfawidhi wa PSPF Mkoa wa Mwanza, Bw. Salim Salum, akitoa rai kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Igaka iliyopo Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza kusoma kwa bidii ili kuinua kiwango cha elimu na kuja kulitumikia Taifa katika siku za baadaye.




Afisa Mfawidhi wa PSPF Mkoa wa Mwanza, Bw. Salim Salumn(wa pili kulia), akitoa elimu kwa kamati ya Shule ya Msingi Igaka iliyopo Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza juu ya Mfuko wa Pensheni wa PSPF na shughuli mbalimbali Mfuko unazofanya ikiwamo kusaidia jamii katika masuala ya elimu, afya, mazingira na maendeleo ya jamii.

 Wanafunzi wa ya Shule ya Msingi Igaka iliyopo Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza wakifurahia msaada wa mabegi ya shule yenye vifaa vya kusomea ulitolewa na Mfuko wa Pensheni wa PSPF.

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Mwanza Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa