WAZEE na walemavu wa viungo wanaoishi katika mazingira magumu katika kambi ya Bukumbi iliyopo Wilaya ya Misungwi mkoani hapa, wamekumbukwa kwa kusaidiwa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya Sh. Milioni 54.
Hafla ya kukabidhi vifaa hivyo ilifanyika jana mbele ya mke wa Rais Dk. John Magufuli, Janet Magufuli katika kambi hiyo yenye watu wenye mahitaji mbalimbali ya kijamii.
Akizungumza wakati akikabidhi vifaa hivyo, Mkurugenzi wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, alivitaja vifaa vilivyotolewa kuwa ni Mchele tani 6, Unga wa mahindi 6, Maharagwe tani 3, Sukari tani 2 na nusu na mafuta ya kula lita 1000.
Dk. Kimei alitaja vifaa vingine vilivyotolewa katika kambi hiyo ya wazee kuwa ni pamoja na umeme wa jua na kudai kwamba hatawataishia hapo wataendelea kutoa misaada ikiwemo kukarabati majengo ya makazi hayo.
Janeth Magufuli
Meneja wa PPF Kanda ya Ziwa, Meshark Bandawe alikabidhi mashine ya kufulia nguo yenye thamani ya shilingi milioni 3 sanjari na kuboresha kituo chao cha madawa ya binadamu yenye thamani ya shilingi milioni 1.5
Mama Janet Magufuli.
Kwa upande wake, Janet Magufuli, alisema kuwa katika kipindi kichache alichozunguka katika kambi 17 nchini alikuta kambi hizo zinakabiliwa na changamoto nyingine ikiwemo ya maladhi.
Alisema kuwa hali hiyo ilisababisha kuanza kutafuta wadau mbalimbali ikiwemo benki hiyo ambayo ilichukua jukumu hilo la kuwasaidia watu hao, wanaokabiliwa na changamoto nyingi.
Mama Janet Magufuli akisalimiana na Meneja wa PPF Kanda ya Ziwa Meshark Bandawe katika ziara yake Kituo cha Bukumbi Mwanza.
Mama Janet Magufuli akisalimiana na Mmoja wa Walezi wa kituo hicho Bw. Juma Makongoro katika ziara yake Kituo cha Bukumbi Mwanza.
Mama Janet Magufuli akisalimiana na Familia na mmoja wa wawakilishi wa familia ya Mbunge wa Misungwi Mhe. Kitwanga, Bi. Magret (kulia) katika ziara yake Kituo cha Bukumbi Mwanza.
Sehemu ya msaada uliotolewa na Benki ya CRDB Mchele tani 6, Unga wa mahindi 6, Maharagwe tani 3, Sukari tani 2 na nusu na mafuta ya kula lita 1000.
Jumuiya ya Kidini ya Wanasaswaminarayan Tawi la Mwanza nao walijumuika katika tukio hilo la kuungana na Mama Janet Magufuli katika kutoa msaada kwa kituo cha Bukumbi.
Mama Janet Magufuli katika picha ya mshikamano na wadau wa Jumuiya ya Kidini ya Wanasaswaminarayan Tawi la Mwanza nao walijumuika katika tukio hilo la kuungana katika kutoa msaada kwa kituo cha kulea wazee cha Bukumbi mkoani Mwanza.
Mkurugenzi wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimeiakisalimiana na wazee na akinamama wanaolelewa ndani ya kituo hicho cha Bukumbi mkoani Mwanza.
Mke wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janet Magufuli akisalimiana na wazee wanaoishi kwenye kituo cha Bukumbi Mwanza.
Kusanyiko lilikutanisha viongozi mbalimbali wa mkoa akiwemo Mweyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama ambaye ni mwenyeji Mkuu wa Mkoa wa Mwanza (kushoto aliyeketi) Magesa Mulongo pamoja na Mbunge wa Jimbo la Ilemela
Kambi hiyo iliyoanzishwa mwaka 1974 kwa sasa ina zaidi ya Wazee 100, kwa muda mrefu sasa watu hao wamekuwa ni omba omba katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Mwanza ambao nao wametengeneza familia kubwa kiasi cha kuanza kutia hofu juu ya hatma maisha ya baadaye.
Wito umetolewa kwa wadau mbalimbali kushirikiana kusaidia kambi hizi, kwa hali na mali ikiwa ni pamoja na ushauri. alisema mama Magufuli.