Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu.
Na:Mhariri; Binagi Blog
Kwa muda mrefu
kumekuwepo na malalamiko kwamba waendesha bodaboda nchini wamekuwa hawatii
sheria za usalama barabarani, hali ambayo imekuwa ikisababisha ongezeko la
ajali zinazoweza kuzuilika.
Hali hiyo
ilimsukuma Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu mwishoni mwa mwezi
uliopita, kutangaza Oparesheni kamata bodaboda wasiotii sheria za usalama
barabara nchini nzima katika kikao kazi kilichowahusisha Maofisa Wakuu wa
Polisi nchini wakiwemo Makanda wa Polisi Mikoa, Vikosi na Makao Makuu, kilichofanyika
Jijini Dar es salaam.
“Pamoja na
kuendelea kudhibiti uhalifu wa aina zote, natoa maelekezo kwa kila Mkoa
kuhakikisha unaendesha oparesheni kali dhidi ya bodaboda ili kupunguza ajali
zinazosababishwa na bodaboda ambao hawataki kufuata sheria na kanuni za usalama
barabarabi”. Alisema IGP Mangu na kuainisha makosa yatakayosababisha bodaboda
kukamatwa kuwa ni pamoja na Kubeba Mishikaki (abiria zaidi ya mmoja), Kutovaa
kofia ngumu (helment) pamoja na kupita katika taa za barabarani huku taa
nyekundu zikiwa zinawaka.
Baada ya
kauli hiyo nilitegemea kuona utekelezaji ukianza mara moja katika mikoa yote
nchini. Lakini hali inaonekana kwenda ndivyo sivyo. Jijini Mwanza, bodaboda
bado makatazo yote ya IGP Mangu yanaendelea kuonekana. Mbaya zaidi ni pale
Binagi Blog inaendelea kushuhudia bodaboda wakipita katika taa nyekundu huku wakiwa
wamewabeba askari wa usalama barabarani.
“Wewe leo
ungekoma. Yaani hawa sijui wakoje. Taa nyekundu zinawaka wao wanapita, tena ona
amembeba askari.” Ilikuwa ni sauti ya malalamiko ya dereva wa daladala moja inayofanya
safari zake za Maduka Tisa-Mzunguko Jijini Mwanza, baada ya kumkosa (nusra
amgonge na gari) dereva bodaboda aliekuwa akipita katika mataa ya barabara ya
Nyerere huku taa nyekundu zikiwa zimewaka, mbaya zaidi akiwa amembeba askari polisi
kikosi cha usalama barabara (alikuwa amevalia sare).
Kwa hali
hiyo, huko ni kumtusi IGP Mangu. Haiwezekani atoe agizo lakini bado agizo hilo
lichukuliwe poa, mbaya zaidi na wale wenye jukumu la kusimamia agizo hilo
(askari wa usalama barabarani). Binagi Blog inahoji “Agizo la IGP Mangu
linatekelezwa au nalo ni kama maagizo mengine ambayo yamekuwa yakitolewa kwa
minajiri ya kuwafurahisha wananchi”?
0 comments:
Post a Comment