Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Katika
ni Robert Paul ambae ni Meneja Masoko ya Kampuni ya Mawasiliano ya TIGO
Kanda ya Ziwa, akizungumza katika zoezi la Utoaji bure wa huduma
mbalimbali za Afya ikiwemo upimaji wa Magonjwa ya Moyo, Utoaji wa
Matibabu kwenye majeraha(Vidonda) pamoja na Uchangiaji damu
lililofanyika juzi jumamosi February 06,2016 katika Uwanja wa Furahisha
Jijini Mwanza.
"Tigo
tumeamua kushiriki zoezi hili ili kuonyesha mfano katika jamii namna
tunavyojumuika na Watanzania katika shughuli za Kijamii, hivyo kupitia
fursa hii ningependa kuwaasa Watanzania kuwa na desturi ya kupima afya
zao mara kwa mara ikiwemo kupima shinikizo la damu, saratani lakini
kubwa zaidi kuwa na moyo wa kujitolea kuchangia damu ili kuwasaidia
wenye uhitaji wa damu. Alisema Paul.
Nae
Cassim Aziz (Kushoto) ambae ni Meneja Masoko wa Tigo Mkoani Mwanza,
alizishauri taasisi pamoja na makampuni mbalimbali nchini kuwa na
desturi ya kushiriki katika shughuli za kijamii hususani kuhamasisha
watanzania kupima afya zao mara kwa mara ili kuepuka athari za kiafya
zinazoweza kuzuilika.
Zoezi
hilo liliandaliwa na Umoja wa Wanafunzi waliosoma Chuo cha Udaktari
Hubert Kairuki cha Jijini Dar es salaam wanaofanya kazi katika Mikoa ya
Kanda ya Ziwa ikiwa ni sehemu ya kuenzi Miaka 17 tangu mwasisi wa chuo
hicho afariki dunia (Februa 06,1999) ikiwa ni miaka miwili baada ya
kuanzisha chuo hicho.
Dkt.Emmanuel
Chacha ambae ni Mkurugenzi wa Hospital ya CJ Jijini Mwanza akizungumza
katika shughuli hiyo ya upimaji wa afya bure ambapo Hospital ya CF
ilikuwa miongoni mwa wadau waliofanikisha shughulio hiyo.
Mwenye
Kinasa Sauti ni Dkt.Francis Tegete ambae ni Mwenyekiti wa Umoja wa
Wanafunzi waliosoma Chuo cha Hubert Kariuki wanaofanya kazi katika Mikoa
ya Kanda ya Ziwa, akizungumza katika shughuli hiyo.
Profesa Paschalis Rugarabamu ambae ni Mlezi wa
Umoja wa Wanafunzi waliosoma Chuo cha Hubert Kariuki wanaofanya kazi
katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa, akizungumza katika shughuli hiyo.
Picha
ya Pamoja ya wa Umoja wa Wanafunzi waliosoma Chuo cha Hubert Kariuki
wanaofanya kazi katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa, akizungumza katika
shughuli hiyo.
Wadau waliofanikisha zoezi la Upimaji afya bure wakiwa katika Picha ya Pamoja ya wa
Umoja wa Wanafunzi waliosoma Chuo cha Hubert Kariuki wanaofanya kazi
katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa, akizungumza katika shughuli hiyo.
Kampuni ya Mawasiliano Tigo ikiendelea na Utoaji wa Huduma zake za Simu kwa wateja
Mmoja wa Wateja wa Kampuni ya Mawasiliano Tigo akipatiwa huduma na wahudumu wa Kampuni hiyo.
Wanafunzi na Wananchi mbalimbali walijitokeza kupima bure afya zao
Zoezi la Upimaji na utoaji huduma za afya bure likiwa linaendelea
Bank ya Damu salama Kanda ya Ziwa ikiendelea na zoezi la ukusanyaji damu kutoka kwa wananchi waliokuwa wanajitolea damu.
Katikati
ni Alfredy Chibuae ambae ni Kaimu Mkurugenzi wa Taaisi ya Tanzania
Rural Health Movement akifuatilia utoaji wa huduma unavyoendelea.
Taasisi hiyo inashughulika na utoaji wa huduma za afya bure kwa watu
wasiojiweza hususani watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi
(mitaani) pamoja na utoaji wa huduma za dharura ikiwemo wale wanaopata
ajali. Taasisi hiyo inapatikana Bugando Jijini Mwanza.
Imeandaliwa na George Binagi-GB Pazzo wa Binagi Media Group
0 comments:
Post a Comment