Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Misasi, Ernest Msiba
akikijaribu kimoja kati ya vitanda 20 kabla ya Waziri wa Mambo ya Ndani
ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza,
Charles Kitwanga (watatu kushoto) kumkabidhi vifaa hivyo Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Nathan Mshana (wapili kushoto).
Waziri Kitwanga alikabidhi vitanda (20), magodoro (20) pamoja na shuka
(20) kwa ajili ya Kituo cha Afya cha Misasi pamoja na vitanda sita kati
ya hivyo walikabidhiwa Zanahati ya Nyamijundu iliyopo Kata ya Kasololo
jimboni humo. Hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika katika Kijiji cha
Misasi. Kushoto kwa Waziri ni Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Kanda
ya Ziwa, Meshack Bandawe, ambapo shirika lake pia lilitoa baadhi ya
misaada katika kituo hicho cha afya. Picha zote na Felix Mwagara.
Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Kanda ya Ziwa, Meshack Bandawe
(kushoto) akimkabidhi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni
Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga, magaodoro
(20) na shuka (20) vyenye thamani ya shilingi milioni tatu na laki tano
katika hafla iliyofanyika Viwanja vya Kituo cha Afya Misasi, wilayani
Misungwi. Waziri Chikawe baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo alivikabidhi
kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, pamoja na vitanda
(20) vyenye thamani ya Shilingi milioni 16 ili aweze kuvigawa kwa Kituo
cha Afya cha Misasi pamoja na Zahanati ya Nyamijundu iliyopo Kata ya
Kasololo jimboni humo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la
Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga akikata utepe wakati akifungua
jiwe la msingi la ujenzi wa Shule ya Msingi ya Ihelele iliyopo Kata ya
Ilujamate, jimboni humo wakati alipofanya ziara ya kutembelea miradi ya
maendeleo pamoja na kuzungumza na wananchi wa eneo hilo. Waziri Chikawe
katika hotuba yake, aliwaahidi wananchi wa eneo hilo upatikanaji wa maji
hivi karibuni kwani eneo hilo linamradi mkubwa wa maji wa Mamlaka wa
Maji Safi na Usafi wa Mazingira Kahama Shinyanga (KASHWASA), hivyo ni
lazima maji yasambazwe kwa vijiji vyote vya jirani.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la
Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga akipanda mti wa kumbukumbu
katika eneo la Shule ya Msingi ya Ihelele iliyopo Kata ya Ilujamate,
Wilaya ya Misungwi. Shule hiyo inajengwa kwa nguvu ya wananchi pamoja na
kuchangiwa na Mamlaka wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira Kahama
Shinyanga (KASHWASA) ambayo inamradi mkubwa wa maji katika Kijiji cha
Ihelele ambapo shule hiyo inapojengwa.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la
Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga akizungumza na wananchi wa Kata
ya Misasi mara baada ya kukabidhi vitanda (20), magodoro (20) pamoja na
shuka (20) katika Kituo cha Afya cha Misasi wilayani Misungwi. Waziri
Chikawe katika hotuba yake aliwaahidi wananchi wa eneo hilo ujenzi wa
barabara ya lami pamoja na upatikanaji wa maji.
Mkuu wa Polisi Wilaya ya Misungwi (OCD), Sylivester Ibrahim akijibu
maswali ya wananchi wa Kata ya Misasi kuhusu usalama katika eneo lao.
Ofisa huyo wa Polisi alipewa nafasi na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles
Kitwanga (kulia-aliyekaa) baada ya wananchi hao kutaka kujua masuala ya
haki zao waendapo Kituo cha Polisi kuripoti matukio mbalimbali.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la
Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga akizungumza na waandishi wa
habari mara baada ya kukabidhi misaada mbalimbali ikiwemo vitanda (20),
magodoro (20) pamoja na shuka (20) katika Kituo cha Afya cha Misasi
wilayani Misungwi
0 comments:
Post a Comment