Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
NA PETER FABIAN, MWANZA.
MKUU wa
Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza, Manju Salum Msambya, amemuagiza
mfanyabiashara maarufu Jijini Mwanza, Kitano Chacha, kuwasilisha vibali
na nyaraka ambazo zinaonyesha uhalali wake kuendelea kujenga ghorofa zaidi ya saba eneo la Mwaloni Kirumba huku akiwa ndani ya mita 60 kinyume na sheria za mazingira.
Msambya
alitoa agizo hilo mwishoni mwa wiki wakati alipofika eneo la Mwaloni
kujionea uharibifu wa barabara inayoelekea Soko la Kimataifa la Mwaloni
Kirumba uliosababishwa na mvua zilizonyesha mfululizo tangu Desemba 22
mwaka jana na kusababisha athari kwa watumiaji wa barabara iendayo Soko
la Kimataifa la Kirumba kutopitika kirahisi ikiwemo magari makubwa ya
mizzigo kunasa kwenye tope.
Akiwa
katika eneo hilo la mwaloni huku akiongozana na Mkurugenzi wa Manispaa
ya Ilemela, John Wanga, alipokea baadhi ya malalamiko ya wananchi na
wafanyabiashara juu ya kero ya barabara hiyo kutopitika kirahisi pia
kudaiwa uharibifu huu pia kuchangiwa na mfanyabiashara Kitano kwa
kumwaga vifusi vya mchanga ambao baada ya mvua kunyesha zikawa tope.
“Tayari
tumekubaliana na Mkurugenzi wa Manispaa, Wanga, kuanza kuifanyia
matengenezo ya dhalula wakati pia tukisubilia mvua ziishe na hatua za
ukaguzi zilizofanywa na wataalam wa Wizara ya TAMISEMI waliofika
kufanya tathimini ya uharibifu ulitokana na mvua zilizonyesha mfululizo
kuanzia Desemba 22 mwaka jana, pamoja na kusubilia ripoti ili kuruhusiwa
kufanya ukarabati hali hii inatulazimu kufanya ukarabati wa
dhalula,”alisema.
Mkuu
huyo wa Wilaya alieleza kuwa watu ambao wamejenga katika kandokando ya
Ziwa Victoria bila kuzingatia sheria za mazingira, vibali halali na
kuamua kujenga kwa jeuri wakitumia fedha zao kupata hati na vibali
kinyume kanuni, taratibu na sheria tumeomba mwongozo wa wataalamu wa
Mazingira (NEMC) kuja kufanya ukaguzi na kutoa maelekezo.
“Hapa
Mwaloni kuna jengo la ghorofa zaidi ya saba linajengwa na ujenzi wake
ni zege tupu ni mali ya mfanyabiashara Chacha nimemuagiza badala ya
kuendelea kujenga alete nyaraka zake za umiliki wa eneo hilo, vibali vya
ujenzi na maelezo kwa nini anajenga jengo hilo ambalo ukiliangalia liko
ndani ya mita 60 ambazo kisheria ni kosa, pia nasikia anasomba mchanga
ili kujaza ziwani ili kupata mita hizo 60 ikibainika tumeomba asifanye
hivyo na akikaidi tutachukua hatua ikiwemo na majengo mengine eneo hilo
la mwaloni,”alisisitiza.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Manispaa, Wanga alieleza kwamba kutokana na
uharibifu wa barabara nyingi za Manispaa kuharibika bado wanaendelea
kusubilia ripoti ya wataalamu wa Wizara ya TAMISEMI kuirejesha
ili kutuwezesha kufanya ukarabati wake lanini kwa hii ya mwaloni tumeona
tuifanyie matengenezo ya dhalula ili kuwezesha kupitika kilahisi.
“Barabara
hii inakwenda kwenye chanzo kikuu cha mapato ya Manispaa yetu ambacho
ni Soko la Kimataifa Kirumba Mwaloni hivyo imetulazimu kufanya ukarabati
wa dhalula na tutatumia zaidi ya Sh milioni 5 kwa kutandaza mawe na
kicha kuweka moramu, barabara za Sabasaba-Kiseke, Kirumba-Ibanda,
Pansiasi-Lumala, Bwiru zinasubilia ripoti ya wataalam wa TAMISEMI,
juu ya waliojenga maeneo yenye utata kwenye fukwe za Ziwa Victoria
tunasubilia pia watu wa Mazingira waje kufanya ukaguzi na kutoa
maelekezo ,”alisema.
CHANZO G SENGO
0 comments:
Post a Comment