Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Ester Bulaya ni Mbunge halali Bunda -Mahakama
Na Blogs za Mikoa
Mahakama kuu kanda ya Mwanza imetupilia mbali kesi ya uchaguzi ya kupinga ubunge wa Bunda mjini na kumpa ushindi Ester Bulaya kutokana na walioleta maombi kutokidhi vigezo vya kisheria vya kufungua kesi.
Kesi hiyo ya madai ilifunguliwa Novemba 19, mwaka 2015 na Magambo Masato na wenzake ikipinga matokeo yaliyompa ushindi bulaya pamoja na wenzake 20 akiwamo mkurugenzi wa wilaya ya Bunda ambaye alikuwa msimamizi wa uchaguzi na mwanasheria mkuu
Baada ya Mahakama kutupilia mbali kesi hiyo Mbunge huyo wa Bunda Mjini Ester Bulaya amesema alishinda uchaaguzi kwa halali na sasa yupo tayari kuendelea na majukumu ya kuwatumikia wananchi.
"Nilimshinda Wasira kwa wananchi, na leo nimemshinda kisheria, Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza imetupilia mbali kesi ya Uchaguzi dhidi yangu, iliyofunguliwa na wapambe wa wasira. Mungu husimama na watu waliowema. Nakutumaini mungu wangu na wewe ndiye mlinzi wangu''
''Asante sana Wananchi wangu wa Bunda Mjini mliokwenda Mwanza kusikiliza Hukumu. Mbunge wenu nipo Dodoma tayari kwa kuanza vikao vya Bunge Kesho"
0 comments:
Post a Comment