Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mwanasheria wa tume ya uchaguzi Bw.Mtibora Seleman akifafanua jambo
wakati wa semina hiyo.
Wanasemina
wakifatilia kwa karibu mafunzo hayo yanayofanyika katika ukumbi wa ofisi ya
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.
Wanasemina
ya masuala ya Uchaguzi kanda ya ziwa wakiwa darasani.
Bi.
Jescar Mongi kutoka tume ya uchaguzi hapa akionesha mfano wa utaratibu wa
upigaji kura utakavyokuwa.
Na Mwandishi Wetu, Kanda ya Ziwa
Imefahamika kwamba maandalizi
muhimu ya uchaguzi mkuu kwa mikoa ya kanda ya ziwa yanaendelea vizuri huku,
waratibu wa uchaguzi, wasimamizi na maafisa uchaguzi kutoka mikoa ya Mwanza na
Mara wakiaswa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu wakati wa zoezi la mchakato
kuelekea Octoba 25 mwaka huu ili kuepusha malalamiko yanayoweza kujitokeza mara
baada ya uchaguzi kumalizika.
Akizungumza wakati wa
ufunguzi wa Semina ya siku mbili iliyo andaliwa na Tume ya taifa ya uchaguzi na
kuhusisha Waratibu wa uchaguzi wa mikoa, wasimamizi wa uchaguzi, wasimamizi
wasaidizi, na maafisa uchaguzi kutoka katika mikoa ya Mwanza na Mara Kaimu mkuu
wa mkoa wa Mwanza Manju Msambya, amesema watumishi hao wanayo dhima ya
kuhakikisha zoezi la uchaguzi linakwenda vizuri kuanzia mwanzo hadi mwisho.
Msambya amesema nilazima
dhamana waliopewa watumishi hao watambue ni muhimu kwakua
inakwenda kutoa mustakabali wa taifa letu na wapi tunako taka kuelekea kwa
kuchagua viongozi kwa nafasi za udiwani, ubunge na urais. “Ndugu wanasemina
tambueni kwamba, madhumuni ya semina hii nikuwajenge uwezo katika mchakato
mzima wa uteuzi wa wagombea, upigaji kura, kuhesabu, kujumlisha pamoja na
kutangaza matokeo ya uchaguzi” hivyo suala la umakini ni muhimu sana.
Msambya amesema, kwakutumia uzoefu
walionao watumishi hao katika mazoezi mbali mbali ya kitaifa wataweza kufanya
kazi hiyo kwa ufanisi mkubwa hasa ikizingatiwa kwamba wengi wao walishiriki
katika zoezi kama hilo kwa mwaka 2010.
Awali akimkaribisha kufungua
semina hiyo Mratibu wa uchaguzi wa kanda ya ziwa Deogratius Nsanzugwanko
alisema tayari maandalizi kadhaa kuhusiana na uchaguzi yamekwisha kamilika
ikiwapo madaftari ya mikoa ya kanda ya ziwa pamoja na vifaa vyote muhimu kuwa
tayari vimekwisha anza kusafirishwa kwenda kwenye mikoa husika.
Kanda ya ziwa inayoundwa na
mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Geita, Kagera, Simiyu na Mara, ambapo kwa mkoa wa
Mwanza pekee inakadiriwa kuwa na wapiga kura 1,442,391 sawa na asilimia 103% ya
lengo lililokuwa limewekwa hapo awali na bodi ya takwimu ya mkoa wa Mwanza ya
kuandikisha wapiga kura 1,403,763.
Imeandaliwa Na: Atley Kuni- The Power of
Media grew.
0 comments:
Post a Comment