Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Waziri wa
Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu aki mkabidhi tuzo maalum ya
heshima Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerari Sarakikya akiwa na mkewe kwa
kupanda mlima Kilimanjaro mara 38, Jenerari Sarakikya pia amepewa Kadi
maalum ya kuingia mbuga zozote za TANAPA Bure yeye pamoja na familia
yake lakini ambapo katika hatua nyingine atalipiwa gharama zote za
kushiriki mkutano wa masuala ya utalii kuhusu milima mirefu zaidi
duniani yeye pamoja na mke wake huko nchini Marekani, Katika mkutano
huo Jenerari Sarakikya anatarajiwa kutoa mada kuhusu mlima Kilimanjaro.
Jenerari
Mrisho Sarakikya amekabidhiwa tuzo hiyo katika hafla ya utoaji wa tuzo
za TANAPA za waandishi wa habari za utalii iliyofanyika kwenye hoteli
ya Gold Crest jijini Mwanza usiku wa kuamkia leo ambapo waandishi wa
habari kutoka vyombo mbalimbali wamepewa tuzo hizo.
Katika
picha kushoto ni Dr. Allan Kijazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi
za mbuga za Taifa TANAPA.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-MWANZA)
Waziri
wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akizungumza katika hafla ya
utoaji wa tuzo za TANAPA za waandishi wa habari kwenye hoteli ya Gold
Crest jijini Mwanza usiku wa kuamkia leo.
Waziri
wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu katikati, Dr. Allan Kijazi
Mkurugenzi wa TANAPA na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii
Dkt. Adelhelm Meru wakiwa katika hafla hiyo iliyofanyika jijini Mwanza
kwenye hoteli ya Gold Crest.
Dr. Allan Kijazi Mkurugenzi wa TANAPA akizungumza katika hafla hiyo.
Waziri
wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu wa pili kutoka kulia akiwa
na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhelm Meru wa
tatu kutoka kulia, Kutoka kushoto ni Devotha Mdachi Kaimu Mkurugenzi wa
(TTB), Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Ndugu Baraka Konisaga na Kushoto ni
Mkurugenzi wa TANAPA Dr. Allan Kijazi.
Theophil
Makunga Mhariri Tendaji wa Jambo Leo akisoma jina la mmoja wa washindi
katika hafla hiyo, Kutoka kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Mh.
Baraka Konisaga na Mkurugenzi wa TTB Bi. Devotha Mdachi.
Waziri wa
Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akikabidhi tuzo kwa Humphrey
Mganga mwandishi bora wa habari za utalii katika magazeti katikati ni
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhelm Meru na
kushoto ni Dr. Allan Kijazi Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA.
Waziri
wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akikabidhi tuzo kwa Fredy
Sikagonamo mwandishi bora wa habari za utalii vipindi vya redio
katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhelm
Meru na kushoto ni Dr. Allan Kijazi Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA.
Waziri
wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akikabidhi tuzo kwa Magessa
Maggesa mwandishi bora wa habari za utalii kwa vipindi vya Televisheni
kutoka Stars TV katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii
Dkt. Adelhelm Meru na kushoto ni Dr. Allan Kijazi Mkurugenzi Mkuu wa
TANAPA.
Waziri
wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akikabidhi tuzo kwa Jimmy
Mengere kutoka Chanel Ten Morogoro mwandishi bora wa habari za utalii
kwa habari za Utalii aliyeandika kuhusu wanyama wanavyouwawa kwa ajali
katika mbuga ya Mikumi.
Waziri
wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akikabidhi tuzo kwa Kasilda
Mrimila Mwandishi bora wa habari za utalii za Televisheni kutoka Star TV
Morogoro kwa kuandika kukauka kwa mto Ruaha Mkuu , kulia ni Mkuu wa
wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga, katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara
ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhelm Meru na kushoto ni Dr. Allan Kijazi
Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA.
Waziri
wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akikabidhi tuzo kwa Jackson
Kalindimya Mwandishi bora wa habari za Utalii Magazeti katikati ni
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhelm Meru na
kushoto ni Dr. Allan Kijazi Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akikabidhi tuzo kwa Frank Leonard
Baadhi
ya wakuu wa vitengo wa mamlaka ya hifadhi za taifa TANAPA wakiwa katika
hafla hiyo kulia ni Mkuu wa Mawasiliano Pascal Shelutete na na wa pili
ni Ibrahim Mussa Mkurugenzi wa Masoko na Utalii TANAPA.
Waziri
wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu katikati akiwa na viongozi
wengine katika hafla hiyo kulia ni Dr. Allan Kijazi Mkurugenzi Mkuu wa
TANAPA , kutoka kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Mh. Baraka
Konisaga na katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii
Dkt. Adelhelm Meru.
Meneja wa Mawasiliano TANAPA Bw. Pascal Shelutete akitoa utaratibu wa utoaji wa tuzo hizo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhelm Meru akitambulishwa katika hafla hiyo.
Mkuu wa Majeshi mstaafu Jenerari Mrisho Sarakikya na mkewe wakitambulishwa katika hafla hiyo.
Mwimbaji Mariam akitumbuiza katika hafla hiyo
Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Mh. Baraka Konisaga akizungumza katika hafla hiyo
Jaji mkuu wa tuzo hizo Dkt. Ayoub Rioba akitambulisha majaji wenzake waliofanya kazi ya kutafuta washindi wa tuzo hizo.
Wanenguaji wa bendi ya Utalii wakitumbuiza katika hafla hiyo
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akipiga picha ya pmaoja na washindi.
0 comments:
Post a Comment