Home » » STADI ZA MAISHA KINGA DHIDI YA MAAMBUKIZI YA UKIMWI.‏

STADI ZA MAISHA KINGA DHIDI YA MAAMBUKIZI YA UKIMWI.‏

 Washiriki mbalimbali wa warsha kuhusu Stadi za Maisha wakimskiliza kwa makini Kaimu katibu Tawala mkoa wa Mwanza Bw.Ndaro Kulinjirwa(hayupo pichani) wakati alipokuwa akizungumza nao leo jijini Mwanza.Bw Kulinjirwa aliwasisitiza washiriki hao kutumia vyema mafunzo watakayopata ili kubadili maisha yao na ya jamii nzima kwani Stadi za Maisha ndio kinga dhidi ya maambukizi ya Ukimwi.
 Mtaalamu wa Stadi za Maisha Bw.Robert Semkiwa(Aliyesimama) akifurahia jambo na washiriki wa warsha ya siku nne kuhusu Stadi za Maisha  kutoka katika mikoa ya Mwanza,Simiyu na Shinyanga leo hii jijini Mwanza.Warsha hiyo imeanza leo ikiwashirikisha Waratibu wa Ukimwi,Maafisa Vijana na Wadau Mbalimbali.Warsha hii inafanyika katika hoteli ya Midland jijini Mwanza.
 Kaimu katibu Tawala mkoa wa Mwanza Bw.Ndaro Kulinjirwa akiongea na Maafisa Vijana,Waratibu wa Ukimwi na Vijana (Hawapo Pichani) kutoka katika Mikoa  ya Simiyu,Shinyanga na Mwanza alipokuwa akizindua rasmi warsha kuhusu Stadi za Maisha kwa washiriki hao leo jijini Mwanza ikishirikisha wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo na Tume ya kudhibiti Ukimwi Tanzania .Warsha iyo ya siku nne  inafanyika katika hoteli ya Midland. Kushoto kwake  ni Mratibu wa Vijana kutoka Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania Bi,Grace Kessy na wa kwanza kulia ni Mtaalamu wa Stadi za Maisha  Bw.Robert Semkiwa.

 Waratibu wa Ukimwi,Maafisa Vijana na Vijana wakiwa katika Picha ya pamoja na Kaimu Katibu tawala Mkoa wa Mwanza Bw.Ndaro Kulinjirwa(aliyekaa mwenye suti ya khaki),Mtaalamu wa Stadi za maisha Bw.Robert Semkiwa(wa Kwanza kushoto aliyekaa),Bi Grace Kessy kutoka Tume ya kudhibiti ukimwi Tanzania  (wa pili kutoka kulia waliokaa) na Bw, Godfrey Masawe ambaye ni Afisa Vijana kutoka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo(wa kwanza kutoka kulia waliokaa).


Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Mwanza Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa