CHAMA cha Mapinduzi (CCM) Taifa, kimesema kwamba hakijachelewa mchakato wa kumtoa na kumtangaza mgombea wake wa Urais kutokana na kuwa na muda wa kutosha wa kufanyakazi hiyo.
Pia kimemtaka Katibu Mkuu wa Chama cha Demkorasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilbrlod Silaa, kuacha kuwapotosha watanzania juu ya zoezi la uwandikishaji wa daftari la kudumu litakalotumika na Tume ya Uchaguzi (NEC) katika uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu ni vyma “Babu” huyo ameanza kuchoka hata kufikiri ni vyema akapumzika siasa.
Akizungumza na waandishi wa Habari katika uwanja wa ndege wa Mwanza, Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM taifa, Nape Nnauye, alisema kwamba kuanzia mwaka 1995, 2000, 2005 na 2010 Chama hakikuwahi wala kuchelewa, kiliweza kumpata mgombea ndani ya wakati na muda sahihi na atapimwa na watanzania kabla ya kumchagua.
“Ni kweli kumekuwa na presha kwa watu wengi ambao wamekuwa wakisema hivyo kuwa tumechelewa kufanya mchakato na kumtangaza mapema mgombea wao, tunacho wahahidi watanzania kuwa hatutachelewa na tutawaletea mgombea ambaye akitangazwa na CCM pale Mjini Dodoma ndiye Rais wa awamu ya tano hivyo wavute subila muda si mrefu vikao vitafanya kazi hiyo,”alisisitiza.
Nnauye alisema kwamba Dk. Silaa hana budi kujitazama upya juu ya mwenendo na matamko yake na kuiachia jukumu la uandikishaji wa daftari la kudumu NEC kwani tume hiyo ni9 huru kufanya kazi yake hiyo , ikiwemo kuanzia mikoa yoyote ya Tanzania ambayo itaona inafaa kutokana na ratiba iliyojiwekea bila kufuata kupangiwa na vyama vya siasa ikiwemo CCM.
“Kabla ya tume kuanza zoezi hilo vyama vyote vya siasa vilikaa na tume na kuelezwa kuanza kwa zoezi hilo na halikuwaeleza kuanzia mikoa ipi, bali vyama viliomba kila raia mwenye sifa ni vyema akaandikishwa katika daftari hilo, sasa inashangazwa na kauli za Dk Silaa kuanza kuilaumu na kuingilia kazi za tume,”alisema.
Katibu huyo alisema kwamba kutokana na wingi wa vijana waliishauri tume kuweka utaratibu mzuri ili vijana wengi wajiandikishe na kuhakikisha inaondosha mizengwe ya kutowapa nafasi katika zoezi linaloendelea katika mikoa ya Rukwa, Njombe na Iringa.
“Kwenye hili CCM tulisema hakuna njia ya mkato watu wote waandikishwe na katika daftari hilo ili kuwawezesha kupiga kura wakati wa uchaguzi mkuu na huo si msimamo wa CCM tu bali vyama vyote vya siasa viliomba kwa NEC, sasa inashangazwa kauli za Dk. Silaa kuwa tume imeanzia zoezi hilo kwenye mikoa ambayo ni ngome yake ili kuudhoofishwa upinzani, si kweli huko ni kuweweseka,”alisema.
Nnauye alisema kuwa CCM haiku kuipangia tume utaratibu na kuingilia zoezi hilo na badala yake inawasisitiza wananchi kujitokeza kujiandikisha katika daftari hilo la kudumu na hakuna njia ya mkato juu ya kujiandikisha, ni vyema pia watanzania wakaepuka poropoganda za viongozi wa kisiasa wanazotumia kuwahadaa.
Aliongeza kuwa Dk. Silaa awaeleze ukweli watanzania juu ya kukaa kwao yeye, Mwenyekiti wa Chadema taifa, Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia na wengine wanaotoka mikoa ya Kaskazini na kuwatenga Mwenyekiti wa CUF, Porfesa Haruna Lipumba na Mwenyekiti wa NRD, Emanueli Makaidi walio kwenye muungano wa Ukawa.
“Waache kuwachochea wananchi na kuwahadaa, CCM itawashinda tu, hivyo ni vyema wakaaacha kuwagawa watanzania kwa uroho wa madaraka wanachotakiwa kujua ni nini watanzania wanataka kupitia sera za vyama vyao na kuacha kuwajaza hasira wananchi kwa madai ya NEC kupendelea maeneo fulani hii si sawa, badala pia kuwajengea hofu,”lisisitiza.
Nnauye pia amemtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Ernest Mangu na vyombo vya vingine vya Ulinzi na Usalama kuvishughulikia vyama vya siasa vinavyoanzisha vikundi kwa kutumia vijana kwa ulaghai wa kuanzisha vikundi hivyo kwa lengo la kujilinda, kwamba CCM inaendelea kurahani vyama vinavyoanzisha vikundi hivyo na vya kiharakati vinalengo la kufanya ugaidi na fujo ni vyema vikadhibitiwa mapema kabla ya kuleta machafuko.
“Isifananishwe Chipukizi na Green Gard wa Chama hicho na vikundi vyao vya kigaidi kwani CCM inao utaratibu mzuri na unaokubalika kwa kuwalea vijana wakiwa wadogo na kuwatumia katika haraiki na gwalidea kwenye sherehe zake na ieleweke kuwa haiandai vikundi vya kupambana na kujilinda kwani kazi hiyo itafanywa na vyombo vya ulinzi na usalama,”alisisitiza.
Kuhusu CCM kukisaidia Chama cha ACT Wazalendo, Katibu huyo aling’aka na kusema kwamba Chama hicho kisihusishwe na migogoro na uchu wa madaraka katika vyama vya upinzani vinavyofarakana wakati huu, lakini pia viache kutumia mbinu ya kujimaliza kwa kutumia mgongo wa Chama kilichopewa dhamana na watanzania kuongoza nchi.
“Wasituhusishe na siasa zao ambazo karibu vyama vyote vya siasa vilivyo kwenye muungano wa Ukawa na vilivyo kwenye usajili, kugombana na kufukuzana kutokana na uchu wa madaraka hivyo ni vyema pia watanzania wakavipima na mwisho kuvinyima kura kwa kuwa haviko tayari kuwatumikia zaidi ya viongozi wake walio wengi kusaka tonge tu,”alisisitiza.
Wito wangu kwa watanzania tudumishe muungano na umoja wa taifa letu bila kubaguana kwa Itkadi zetu za vyama vya siasa na tuhakikishe kila mtanzania awe ni mlinzi, kuwa na taifa lenye machafuko ni kuwafanya watu wawe wakimbizi kudadumaza ustawi wa taifa chini ya mfumo wa vyama vingi na wanaotaka kuwagawa kwa manufaa ya kupata madaraka tusiwaunge mkono kamwe.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment