Tone

Tone
Home » » WANNE WAUAWA KWA TUHUMA ZA WIZI

WANNE WAUAWA KWA TUHUMA ZA WIZI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

WATU wanne wameuawa kwa kupigwa marungu, kuchomwa mikuki na miili yao kuteketezwa kwa moto wilayani Sengerema, Mwanza wakituhumiwa kuwa wezi.
Watu hao huku wawili kati yao ni ndugu, waliuawa na wananchi  wa kijiji cha Iyogelo, Kata ya Buzilasoga, wilayani Sengerema wakishirikiana na walinzi wa maduka wa eneo hilo.
Vijana hao waliuawa muda mfupi baada ya kutoka disko ambapo watatu kati yao walichomwa moto na kubaki majivu huku mmoja aliyekuwa amechomwa mkuki na kufanikiwa kukimbia akifia katika hospitali Teule ya Wilaya ya Sengerema alikokuwa akipatiwa matibabu.
Tukio hilo lilitokea Oktoba 26 mwaka huu, saa nane usiku wakati vijana hao wakitoka kwenye ukumbi wa disko uliopo maeneo hayo.
Waliouawa ni Faustine Kazungu (22), Kweli Thobias (22) na mdogo wake Kahangala Thobias (20), wote wakazi wa kitongoji cha Igogo A, Kata ya Nyampulukano.
Mwingine ni Bahati Misalaba(22)ambaye katika purukushani hizo alifanikiwa kukimbia akiwa amechomwa mkuki wenye sumu kiunoni na kufariki dunia akiwa hospitali Teule ya Sengerema.
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Nyamazugo Road, Buluma Buluma, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwataka wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi.
Mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai Wilaya ya Sengerema (OCC-ID), John Lwamlema, mbali na kusikitishwa na mauaji hayo, alivitaka vyombo vya habari kuwa mstari wa mbele kuielimisha jamii kuacha kuuwa watu, kwani kwa kufanya hivyo ni kutenda kosa la jinai.
CHANZO:TANZANIA DAIMA

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mwanza Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa