Kampuni ya Msama Promotions Ltd,kwa kushirikiana na Wizara ya habari vijana,utamaduni na michezo imetangaza neema kwa wasanii kuanza zoezi la kuwakamata watu wanaouza nakala feki za wasanii hapa nchini.
Mkurugenzi wa kampuni hiyo,Bwana Alex Msama amesema hayo jijini dar ,kuwa zoezi hilo limekwishaanza, na mpaka sasa wamekamatwa vijana wane katika mkoa wa Dodoma na watatu jijini Mwanza.
‘’Kuna kazi mbalimbali ambazo zinaibiwa kila kukicha huku wamiliki wa kazi hizo wakiendelea kushuka kiuchumi na kutoona faida yoyote
ya kazi hizo,huu ni wakati kwa wasanii kuneemeka na kazi
zao.Hivyo tutahakikisha tunafika kila mahali hata sehemu zisizofikika
kirahisi na yote hii ni kuonyesha kuwa tunajali na tunathamini kazi za
wasanii wetu’’,alisema Msama kwa msisitizo.
Alisema, nakala zote zitakuwa na stika za TRA kuhakikisha hakuna wizi wowote unaofanyika na
unaotokea katika kazi mbalimbali za wasanii.Stika hizo zimewekwa ili
kuwabaini wale wote wenye hulka hiyo ya kuiba kazi za wasanii
.Operesheni hiyo itafanyika bila
kujali wadhifa wake ama cheo chake,akaongeza kusema kuwa zoezi hilo ni
salamu kwa wale wote wanoatumia kazi za wasanii bila kufuata utaratibu wa sheria zilizopo.
Pia
amelipongeza Jeshi la Polisi nchini kwa kazi nzuri wanayoifanya katika
kuhakikisha wanatoa ushirikiano wa kutosha katika changamoto,na pia
wamekuwa wakishirikiana nao kuhakikisha zoezi hilo linakuwa endelevu na kuzunguka kila mkoa kuhakikisha kazi za wasanii zinaheshimiwa na zinalindwa kwa kila namna.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment