Home » » HII NI HATARI SANA:WEZI WATATU WA ATM WAKAMATWA MWANZA..SHUHUDIA HAPA

HII NI HATARI SANA:WEZI WATATU WA ATM WAKAMATWA MWANZA..SHUHUDIA HAPA


JESHI
la Polisi mkoani Mwanza kwa kusaidiana na maofisa wa Benki ya NMB
imewatia mbaroni watu watatu ambao wanadaiwa kuiba kiasi cha Sh700
milioni kwa nyakati tofauti.




 Watuhumiwa
hao wamenaswa baada ya kuwekewa mtego na maofisa wa benki na polisi 
kwenye saa 6.00 usiku wa Februari 10, mwaka huu na mtuhumiwa mmoja 
alibambwa akichukua fedha katika ATM ya NMB kwenye Tawi la PPF Plaza 
Mwanza.



Baada ya 

kunaswa kwa mtuhumiwa huyo, alisaidia kuwaelekeza polisi walipo wenzake,
ambao walikutwa katika hoteli moja jijini Mwanza wakiwa wamejipumzisha.
Akizungumza
na waandishi wa habari, Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mwanza,
Christopher Fuime alisema pia walikamata vifaa mbalimbali ambavyo
walikuwa wakitumia kwa ajili ya kufanyia uhalifu huo.

Vifaa walivyokamatwa navyo
Vifaa
vilivyokamatwa navyo ni kadi za bandia 194 za kuchukulia fedha katika
ATM za Benki ya NMB, ambapo kati yake kadi 95 zilikuwa na
namba 0225152975 zinazotumia namba ya akaunti ya 2258103695 zenye jina
na picha ya mtu anayedaiwa kuwa ni mtumiaji mwenye jina la Molely L. P.
Kadi nyingine 99 zilikuwa na namba 0506056317 za akaunti
namba 5068000322 zikitumia jina moja la Mnuo Z. E na picha moja.

Mbali

na kadi hizo pia waliweza kunasa kadi 36 za Benki za DTB, ambazo kati 
yake kadi 18 zilikuwa na jina moja la Kelvin G. Gratias na namba 20497883,
kadi 12 zikitumia jina la John J. Paul zenye akaunti namba 2049783 huku
kadi sita zikitumia jina moja la Joseph Donald akaunti namba 2049783.


Kadi 

nyingine tatu zenye maandishi ya Download List na nyingine ikiwa ni kadi
ya Visa ya Benki ya KCB yenye namba 4183546040003827 zikitumia jina la 
Elikana Zacharia. Kadi nyingine zilikuwa ni tupu zisizo na maandishi 
wala nembo ya benki yoyote na nyingine zikiwa ni Soviet Royalty, kadi ya
raia ya Urusi ikiwa na namba 000724.

Pia walikutwa na kadi ya Benki ya Amerikani yenye namba 549012345678 zilizokuwa zikitumia jina la Richard Croswell.


Walikamatwa

pia wakiwa na vifaa mbalimbali vya kielektroniki ikiwamo kamera za siri
tatu za kienyeji ambazo zimetengenezwa kwa kufungwa betri za simu ya 
mkononi na pia walikamatwa na kifaa cha kutengenezea kadi bandia 
(Magnetic Card reader), mikebe mitatu ya rangi za kupulizia kamera za 
usalama katika ATM ili wasionekane wakati wa wizi wao, ‘printer’ pamoja 
na kifaa cha kuchomea vifaa vya umeme.

Wizi ulivyofanyika
Wahalifu
hufika katika mashine za kutolea fedha ambapo hatua ya kwanza ni kuzima
kamera za usalama za eneo husika kwa kuzipulizia rangi maalumu ili
kuzitia ukungu hivyo kuharibu mwonekano wake na kuruhusu wao kuingia
eneo hilo bila ya kuonekana na kufanya wizi wao.

Mara

baada ya kuziharibu kamera za usalama, walikuwa wakianza kwa kuweka 
kamera zao za siri ili kunasa namba za siri za kufungulia akaunti ambazo
huzisoma katika ‘kompyuta’ na kuzinakili katika daftari lao maalumu na 
kisha kuchukua kadi zao bandia na kuchukua fedha.


Wizi huo 

wa kuchukua fedha waliufanya nyakati za usiku saa sita hadi saa tisa 
usiku wakati ule wa kutegea kamera zao ulifanyika muda ambao huwa na 
wateja wengi hasa siku za mapumziko.
Chanzo Dj Sek Blog

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Mwanza Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa