Home » » WENYEVITI UKEREWE WASUSIA MAENDELEO

WENYEVITI UKEREWE WASUSIA MAENDELEO



na Jovither Kaijage, Ukerewe
SHUGHULI za maendeleo wilayani Ukerewe, Mwanza zimeanza kukwama baada ya wenyeviti wa vitongoji kususa kushiriki na hata kuamasisha wananchi kutojitokeza katika mikutano ya viongozi wakishinikizwa kulipwa posho mbalimbali ikiwamo ya Sensa ya Watu na Makazi.
Msimamo huo umedhihirika juzi baada ya mkutano wa hadhara ulioitishwa na mkuu wa wilaya hiyo katika Kijiji cha Hamkoko kushindwa kufanyika baada ya wenyeviti wa vitongoji kugoma kualika wananchi.
Habari kutoka katika kijiji hicho zinasema pamoja na Ofisa Mtendaji wa Kata ya Ngoma, Khamis Ndaro, kuwaelekeza wenyeviti wa vitongoji kushiriki kikao cha ndani cha viongozi wa vijiji viwili vya Hamkoko na Muluseni pamoja na kualika wananchi kushiriki mkutano wa haadhara, lakini hali ilikuwa tofauti.
Wakieleza sababu ya kususia shughuli za maendeleo kwa nyakati tofauti, wenyeviti hao wanataka kulipwa posho ya sh 50,000 kila mmoja ya kushiriki sensa mwaka huu pamoja na posho ya madaraka ya kila mwezi ya sh 5,000 ambayo haijalipwa zaidi ya miezi tisa sasa.
Mwenyekiti wa umoja wa wenyeviti wa vitongoji katika wilaya hiyo, Hussein Hassan, alisema katika vikao vyao wamekubaliana kutoshiriki shughuli zote za maendeleo hadi madai yao yatakapotekelezwa.
Mkuu wa wilaya hiyo, Mary Tesha, alithibisha mkutano huo kutofanyika kutokana na wananchi kutoalikwa.
Chanzo: Tanzania Daima

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Mwanza Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa