Na Mwandishi wetu
Walimu
wanne wa Shule ya Msingi Hamkoko Wilaya hapa mkoani Mwanza
wanashikiwa na polisi kwa tuhuma ya kukutwa wakiandaa majibu ya
mtihani wa Taifa wa darasa la saba.
Walimu hao walikamatwa na polisi juzi majira ya saa 5.10 asubuhi nyumbani kwa mmoja wa watuumiwa hao wakiendelea na harakati za kuandaa majibu ya mtihani ili kuwasaidia wanafunzi wa shule hiyo.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza , Leberatus Barlow amewataja walimu hao kuwa ni Kija Songoli (30), Jenfrida Edward (28), Merycelina Malisel (25) na Maliam Kateti (26) ambaye alikuwa Msimamizi wa Mtihani huo katika shule hiyo.
Alisema mwalimu Diana Shishangali ambaye ni mmoja wa watuhumiwa anatafuta baada ya kutoka ili aunganishwe na wenzake kwa ajili ya kufikishwa mahakamani.
Kamanda Barlow alisema walimu hao walikutwa nyumbani kwa Kija Songoli wakiwa na nakala ya mtihani wa Hesabu, mashine moja ya kufanyia mahesabu, kalamu pamoja na vipande kadhaa vya kalatasi vikiwa tayari vimeandikwa majibu ya mtihani huo vikiwa vimefichwa chini ya godolo.
Alisema wakati uchuguzi zaidi wa tukio hilo ukiendelea, tayari baadhi ya vielelezo vimepatika na vimeandaliwa ili vipelekwe kwa wataalamu wa kutambua miandiko ili kubaini aliyeusika na kosa hilo.
Kwaupande wake Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Mery Tesha, alisema ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuimarisha ulinzi ili yeyote atakayepatikana kufanya hujuma za kuiba mitihani akamatwena kuchukuliwa hatua kwamujibu wa sheria.

Chanzo: Nipashe
0 comments:
Post a Comment