Na Christopher Gamaina, Mwanza
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza anayemaliza muda wake, Clement Mabina, amejitokeza kuomba ridhaa ya kutumikia nafasi hiyo kwa kipindi kingine.
Hata hivyo, akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuchukua fomu, Mabina alisema amejipanga kukitumikia chama hicho kwa ufanisi mkubwa.
“Bado nina kiu kubwa ya kukitumikia chama, kutokana na uzoefu nilioupata katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, ninaamini sasa utanisaidia kukiongoza chama chetu kwa ufanisi wa hali ya juu.
“Unajua CCM siyo fisadi, lakini Serikali yetu itaendelea kushughulikia viongozi mafisadi chini ya misingi ya sheria na vyombo vya dola kwa jumla,” alisema.
Mabina aliongeza kuwa bado ana shauku ya kujenga umoja na mshikamano wa wanachama wa CCM na kuyajengea makundi mbalimbali ya jamii uwezo wa kiuchumi.
Mabina alisema katika kipindi cha uongozi wake alimshawishi Rais Jakaya Kikwete akakubali kuwapatia wafanyabiashara ndogondogo (machinga) jijini Mwanza msaada wa Sh milioni tano.
Kuhusu nguvu ya vyama vya upinzani, Mabina alisema:
“Nimejipanga kushirikiana na viongozi wengine kuhakikisha tunadhoofisha hoja za wapinzani na kukiwezesha chama chetu kutwaa ushindi wa majimbo katika uchaguzi ujao.
“Tumedhamiria kuendelea kujenga taswira ya chama chetu mbele ya wana Mwanza na Watanzania kwa ujumla ili kudumisha heshima na hadhi ya chama chetu,” alisema.

Chanzo: Mtanzania
0 comments:
Post a Comment