Tone

Tone
Home » » TFS YASAIDIA MADAWATI 12,000 MKOANI MWANZA

TFS YASAIDIA MADAWATI 12,000 MKOANI MWANZA


Naibu Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii , Eng. Ramo Makani( kushoto) akimkabidhi madawati Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela ( kulia) ikiwa ni utekelezaji wa ahadi iliyotolewa bungeni mwanzoni mwa mwaka huu na Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe ya kutengeneza madawati 20,000, wa pili kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo( Picha na Lusungu Helela- Wizara ya Maliasili na Utalii).

Baadhi ya madawati yaliyokabidhiwa jana na Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kwa Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongela ikiwa ni utekelezaji wa ahadi iliyotolewa bungeni mwanzoni mwa mwaka huu na Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe ya kutengeneza madawati 20,000 .
Baadhi ya wanafunzi wakiwa wamekaa kwenye madawati mara baada ya makabidhiano yaliyofanyika Mkoani Mwanzan jana na Naibu Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza , John Mongela ikiwa ni utekelezaji wa ahadi iliyotolewa bungeni mwanzoni mwa mwaka huu na Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe . ( Picha na Lusungu Helela- Wizara ya Maliasili na Utalii)

Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) imekabidhi madawati 12,115 mkoani Mwanza ikiwa ni utekelezaji wa ahadi iliyotolewa bungeni mwanzoni mwa mwaka huu na Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe ya kutengeneza madawati 20,000. Makabidhiano hayo baina ya TFS na Serikali yalifanyika kitaifa kwenye Uwanja wa chuo cha Mafunzo ya Taaluma ya Wanyamapori Pasiansi.

Naibu wa Waziri wa Wizara hiyo , Ramo Makani alitoa mwezi mmoja kwa uongozi wa TFS kuhakikisha unakamilisha kutengenenza madawati 7,885 yaliyosalia kabla ya novemba mwezi huu .‘’ Pamoja na kufikia asilimia 61 ya lengo, nawaomba TFS muhakikishe idadi iliyobaki ya madawati inakamilika ifikapo mwishoni mwa mwezi ujao’’ Alisema Makani.

Akizungumza kabla ya kukabidhi madawati hayo, Mtendaji Mkuu wa TFS, Prof. Dos Santos Silayo bila kutaja gharama iliyotumika alisema ofisi yake imechelewa kufikia asilimia 100 ya kutengeneza madawati 20,000 kutokana na kuwa na changamoto ya ucheleweshwaji wa taratibu za uvunaji mbao katika baadhi ya misitu.

TFS tumetekeleza agizo hili kwa kulenga ngazi za chini kabisa za mfumo wa utendaji wa Wakala ambao ni wilaya. Hivyo katika kugawa idadi ya utengenezaji madawati wa kanda ilizingatia idadi ya wilaya kwa kila kanda’’ alisema Prof. Silayo. Waziri Makani alisema madawati hayo yatagawiwa katika mikoa ya Simiyu., Kagera, Mara,Geita na Mwanza ambayo itapokea madwati 2,580 yaliyokwisha tengenezwa.

Akizungumz kwa niaba ya Wakuu wa Mikoa ya Tanzania Bara, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela aliwapongeza TFS na kuahidi kuyatunza madwati hayo ili yatumike kwa muda mrefu kwa manufaa ya wanafunzi.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mwanza Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa