Na mwandishi wetu, Mwanza
Benki
ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imesema imeridhishwa na
uwekezaji wa Kiwanda cha Nyama cha Chobo kilichombo Misungwi jijini
Mwanza kwa kuwa kinawahakikishia wakulima wadogo masoko ya mifugo yao.
Pongezi
hizo zimetolewa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis
Assenga wakati alipofanya ziara ya kujionea maendeleo ya uwekezaji wa
miundombinu ya Kiwanda hicho.
Bw.
Assenga amesema kuwa Kiwanda cha Chobo ambayo inamilikiwa na kijana
mzalendo, John Chobo ina uwezo mkubwa wa kusadia wakulima wadogo kwa
kununua mifugo yako hivyo kuwapatia fursa za masoko wakulima hao.
“Miundombinu
ya Kiwanda inaweza kuchinja zaidi ya ng’ombe 600 kwa siku, hili ni soko
kubwa sana kwa wakulima wadogo wa mikoa ya Kanda ya Ziwa hali
itakayounga mkono juhudi za serikali hasa TADB katika kuboresha minyororo ya thamani kwenye sekta ya mifugo,” alisema.
Bw.
Assenga amesema Serikali iliamua kuanzisha Benki ya Maendeleo ya Kilimo
Tanzania (TADB) ili kusaidia kukabiliana na mapungufu ya wakulima
nchini kote ili kuhuisha upatikanaji wa mikopo katika sekta ya kilimo na
kuchagiza mapinduzi katika kilimo nchini.
Bw.
Assenga ameongeza kuwa sekta ya mifugo ni mojawapo ya minyororo ya
mwanzo inayopatiwa mikopo kwa ajili ya uongezaji wa thamani mazao na
mifugo mbalimbali hasa katika uongezaji wa thamani wa ufugaji wa ng’ombe
wa nyama na maziwa nchini.
Ameongeza kuwa Benki yake imejipanga kuendeleza uongezaji wa thamani wa Ufugaji wa Ng’ombe wa Nyama na Maziwa.
“Benki
inatoa mikopo na kusaidia uwekezaji kwa ajili ya ujenzi, ununuzi wa
mitambo na ufungaji wa mitambo ya kuhudumia ng’ombe ikiwemo majosho na
mabwawa ya kunyweshea na pamoja na usindikaji wa nyama na maziwa kwa
ajili ya kuongeza thamani nyama na maziwa,” alisema Bw. Assenga.
Akizungumza
wakati wa ziara hiyo, Mmiliki wa Kiwanda hicho, Bw. John Chobo alisema
kuwa kwa sasa kiwanda chake hakijafikia uwezo wa kutumika kwa asilimia
100 kutokana na changamoto za kimtaji zinazomkabili na alitumia fursa
hiyo kuiomba Benki ya Kilimo kumuwezesha ili aweze kutoa ajira zaidi kwa
Watanzania.
Kwa
mujibu wa Bw. Chobo kwa sasa kiwanda chake kina wafanyakazi 85 na
kikifikia uwezo wa kuzalisha kwa asilimia 100 kitaweza kuajiri zaidi ya
wafanyakazi 300 watakaofanya kazi kiwandani na 300 watakaokuwa
wakisimamia shamba.
“Tunaiomba
TADB kutatulia changamoto za ukosefu wa mitaji ya uhakika kwa kuwa kwa
kiasi kikubwa na mikopo mingi kutoka taasisi za fedha kuelekezwa zaidi
kwenye upande wa biashara za bidhaa na ambayo riba yake ni kubwa sana.,”
alisema.
0 comments:
Post a Comment