Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
|
NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said, Mwanza
MAKAMU
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan,
anatarajiwa kufungua rasmi semina kwa wastaafu watarajiwa iliyoandaliwa na
Mfuko wa Pensheni wa PSPF, na kufanyika kwenye ukumbi wa chuo cha mafunzo kwa
watumishi wa Benki Kuu ya Tanzania, (BoT), jijini Mwanza.
Akizungumza
kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, kwenye ufunguzi wa semina hiyo iliyoanza
leo Juni 2, 2017, Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Mfuko huo, Bw. Gabriel Silayo
alisema, semina hiyo inalenga kuwandaa kwa kuwapa mafunzo watumishi wa umma
ambao wanatarajiwa kustaafu hivi karibuni, ili hatimaye wastaafu kwa amani.
“Na
kwa kufanikisha hilo, tunao maafisa wetu watatoa mada mbalimbali, wapo
washirika wetu, SIDO, na mabenki kama vile NMB, CRDB, TPB, MCB na UTT, ambao
watatoa elimu ya namna bora ya kutunza na kutumia fedha zako za mafao.” Alibainisha
Bw. Silayo.
Bw.
Silayo pia alisema, kwa kutambua kipaumbele cha serikali ya awamu ya tano chini
ya uongozi wake, Rais Dkt. John Pombe Magufuli, kauli mbiu ya semina hiyo ni “Mafao
ni Mtaji wa Uwekezaji Sahihi”. “Na ndio maana tumewaleta SIDO hapa ili
wawaelimishe jinsi mtakavyoweza kuanzisha viwanda vidogo vidogo baada ya
kustaafu utumishi wa umma na ndugu zangu napenda niwahakikishie hilo
linawezekana.” Alisema
Alisema
semina hiyo itakuwa ya siku mbili na kwamba, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan ataifungua rasmi kesho Jumamosi
Juni 2, 2017.
Zaidi
ya watumishi 300 kutoka sekta mbalimbali za utumishi wa umma kwenye wilaya zote
za mkoa wa Mwanza wanahudhuria semina
hiyo ya mafunzo.
|
|
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw. Gabriel Silayo, akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina hiyo ya mafunzo kwa wastaafu watarajiwa |
Meneja Pensheni wa PSPF, Bw. Mohammed Salim, akitoa mada juu ya maandalizi na fursa za wastaafu
Afisa Mwandamizi wa Utafiti wa PSPF, Bw. Mapesi Maagi, akigawa vitendea kazi kwa washiriki wa semina mwanzoni mwa mafunzo hayo
Bw. Silayo, (Kushoto), akiteta jambo na Meenja wa Mipango na Utafiti wa PSPF, Bw. Luseshele Njeje.
Mshiriki akizunguzma wakati wa semina hiyo
Afisa Uhusino Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi akitoa utaratibu wa namna semina hiyo itakavyoendeshwa
Mshiriki akinukuu kilichokuwa kikiendelea
Wanasemina wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zikitolewa
Baadhi ya wadau wa PSPF, na washiriki wa semina wakifuatilia mada zilziokuwa zikitolewa
Washiriki wa semina wakiwa kwenye ukumbi wa chuo cha mafunzo BoT jijini Mwanza
Bw. Silayo, (Kushoto), akimsikiliza kwa makini Meneja wa Fedha wa Mfuko huo, Bw.Lihami Masoli
Kuonyesha semina hiyo ilikuwa muhimu kwa wastaafu hawa watarajiwa, mshiriki wa semina akinakili kwa uangalifu mkubwa yaliyokuwa yakielezwa (mafunzo)
Afisa Mfawidhi wa PSPF, mkoani Mwanza, Bw.Salim Salum, akifafanua baadhi ya hoja zilizojitokeza. Kulia ni Mkurugenzi wa Uwekezaji wa PSPF, Bw. Gabriel Silayo na katikati ni Meenja wa Pensheni wa Mfuko huo, Bw. Mohammed Salim
Sehemu ya washiriki wa semina
Mshiriki akipitia ratiba
Washiriki hawa wakipitia vipeperushi vya PSPF vyenye taarifa mbalimbali za Mfuko
0 comments:
Post a Comment