Tone

Tone
Home » » MAJONZI YATANDA STAR TV.

MAJONZI YATANDA STAR TV.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Mwenyezi Mungu daima hakosei, kila afanyalo lina sababu zake kutokea, kazi yake ihimidiwe...kaamua akupumzishe kaka na hii dunia HADAA... Wakuitwa David Ngahyoma alikuwa mfanyakazi wa Star Tv upande wa picha, akimudu vyema uchukuaji wa matukio kwa 'angle adimu'.

Mbali na habari Marehemu David Ngahyoma, pia  alimudu vyema uchukuaji wa matukio ya kutengeneza vipindi, ambapo moja ya vipindi alivyokuwa akiviongoza katika uchukuwaji picha, vikapata sifa kote nchini na nje ya nchi ni kipindi cha ucheshi Star Tv cha FUTUHI.

Utakumbukwa kwa ubunifu wako, Hukusita kusifia pale penye sifa palipo fanya vyema na ukaweka ushauri kuboresha, Kaka umeenda!! Yule uliyependa kuishi vyema na vijana wenzako na ulikuwa msumbufu kuhamasisha ushirikiano.

Kaka nalikumbuka cheko lako nakumbuka ujasili wako...PUMZIKA SALAMA...DAIMA KIVULI KINAISHI...Kivuli chako kitaishi daima dumu... David Ngahyoma..LALA KAKA!

MWEZI MUNGU MWENYE REHEMA TWAKUOMBA UILAZE PEMA PEPONI ROHO YA MAREHEMU DAVID NGAHYOMA. AMEN

KWA HISANI YA G SENGO BLOG

1 comments:

Makome Adarick said...

Bwana ametoa......na ametwaa....jina lake lihimidiwe milele....
Poleni sana wanafamilia na Jamii nzima ya Star tv.....na FUTUHI kwa upekee

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mwanza Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa