Tone

Tone
Home » » MWANZA KU-JEMBEKA NA SAUTI SOL JUMAMOSI HII FEB 21 NDANI YA JEMBE BEACH‏

MWANZA KU-JEMBEKA NA SAUTI SOL JUMAMOSI HII FEB 21 NDANI YA JEMBE BEACH‏

300 x 150m
Hatimaye ule mpango mzima wa kuzifungulia burudani ulioasisiwa na redio mpya ya jijini Mwanza JEMBE FM na kubatizwa jina 'JEMBEKA' unaanza rasmi jumamosi ya wiki hii tarehe 21/02/2015 ndani ya kiota cha burudani cha kitalii Jembe Beach Mwanza.
Burudani itakayo fungua mpango huo wa 'JEMBEKA' ni kutoka kwa kundi maarufu Afrika Mashariki lililovuka mipaka na sasa muziki wake kuchezwa hadi barani Ulaya kundi la Sauti Sol toka nchini Kenya ambao watapiga muziki LIVE.
Vijana wa Nyumbani JJ Band nao watakuwepo ndani ya Jembe Beach Resort kwaajili ya kumwaga burudani ya kijanja zaidi ya vile ulivyowazoea.
Kiingilio ni shilingi 10,000/= kwa tiketi za awali na Tshs 15,000/= ukinunua getini.
Tiketi zinapatikana ofisi za Jembe Fm zilizopo PPF Plaza Mwanza.
Ni chini ya udhamini wa K Vant Gin, Coca cola, ikiwezeshwa na Jembe ni Jembe, Jembe Fm, Jembe Djz na G.SENGO BLOG.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mwanza Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa