Tone

Tone
Home » » WENJE: MSIKUBALI KUCHANGISHWA FEDHA

WENJE: MSIKUBALI KUCHANGISHWA FEDHA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

MBUNGE  wa  Nyamagana kupitia Chama cha Democrasia na Maendeleo (CHADEMA), Ezekiel Wenje, amewashari wananchi mkoani hapa kutokubaliana na uchangishwaji wa fedha na Halmashauri ya Jiji kwa ajili ya ujenzi wa maabara shuleni kwa kuwa fedha za mapato yanayotokanayo na ushuru hufanya kazi hizo.
Wenje, alitoa kauli hiyo jana wakati akiwahutubia mamia ya wakazi ya Kata ya Buhongwa nje kidogo ya Jiji la Mwanza.
Alisema haungi mkono uchangishwaji wa fedha hizo, kwani kuendelea kufanya hivyo ni kuongeza ufisadi unaofanywa na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwa lengo la kujinufaisha binafsi.
“Nikiwi kama Mbunge wa jimbo hili, mimi siungi mkono wananchi kuchangishwa hizo fedha, kwani zinaenda kufanya kazi ambayo haijakusudiwa, kwa hiyo msikubali kuchanga hizo fedha wanazotaka mchange.
Kaya moja inachangishwa sh 5,000 na Mwalimu anakatwa 10,000 kila mwezi na unakuta hajashirikishwa wakati wanafanya mpango huo, na mshahara wake wenyewe ni mdogo, unapomkata kiasi hicho atabaki na nini alihoji,” Wenje.
Wenje, alisema kuna fedha nyingi ambazo zingefanya kazi ya kujenga maabara za kisasa nchi nzima, lakini CCM kinazitumia katika kusherehekea kukubidhiwa kwa rasimu iliyopendekezwa na Bunge Maalumu la Katiba zilizofanyika juzi mkoani Dodoma.
Mbunge huyo, alisema kumekuwepo na vitisho kwa wananchi kutoka kwa baadhi ya viongozi wa Jiji, wakiwalazimisha kuchanga kiasi hicho cha fedha, kitendo ambacho ni kinyume na utaratibu na kuhoji kuwa fedha zinazotokana na mapato ya halmashauri hiyo zinafanya kazi gani.
Ujenzi wa maabara Mkoa wa Mwanza, unahitaji sh bilioni 5 ambazo zinatarajiwa kujenga vyumba zaidi ya 60 na hadi sasa zimepatikana sh bilioni 1 na ujenzi umefikia asilimia 46 kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Hassan Hida.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mwanza Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa