Tone

Tone
Home » » AUAWA KWA KUCHARANGWA MAPANGA

AUAWA KWA KUCHARANGWA MAPANGA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

MKAZI wa Mtaa wa Ihangilo Nyakato jijini Mwanza, Annastazia Crysant (57), ameuawa kwa kukatwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake akiwa nyumbani kwa Sylvester Raphael katika Kata ya Mahina, alikokwenda kujipumzisha baada ya kuandamwa na matukio ya kuvamiwa.
Tukio hilo lilitokea Oktoba 21 mwaka huu saa 7:00 usiku, ambako watu wasiojulikana walivamia nyumbani kwa Raphael na kutenda unyama huo.
Akizungumza na Tanzania Daima, mtoto wa marehemu, Yuritha Simon, alisema kuwa wakati wauaji hao wakiwavamia, alikuwa amelala na mama yake kitanda kimoja.
Alisema kuwa alishtuka ghafla baada ya kusikia kelele, lakini alipoamka alimkuta mama yake amekaa kitandani na alimuuliza kuna nini, akamuonyesha kwa ishara kuwa anyamaze kimya, kwani majambazi walikuwa wamevamia nyumbani hapo.
Kwamba, baada ya muda mfupi wavamizi hao walivunja mlango kwa kutumia jiwe kubwa na kuingia chumba walichokuwa wamelala wawili hao, kisha kuanza kuwashambulia sehemu mbalimbali za miili yao huku wakiomba fedha.
Yuritha, alieleza kuwa mama yake aliwapa sh 15,000 pamoja na simu aina ya Nokia, ndipo wakatokomea kusikojulikana.
Aliongeza kuwa, majirani walifika na kumkimbiza mama yake katika Hospitali ya Bugando kwa ajili ya matibabu, lakini alifariki dunia wakiwa njiani.
Majirani hao, waliliambia gazeti hili kuwa kitendo cha Jeshi la Polisi kushindwa kuyafanyia uchunguzi matukio mawili ya nyuma ambayo marehemu aliwahi kuyaripoti, ndicho kimesababisha kifo chake.
Mtoto mwingine wa marehemu, Siriyako Simon, alisema kuwa mara ya kwanza mama yao alivamiwa na kundi la watu wanaodhaniwa kuwa ni vibaka na kukatwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake na kisha kumpora sh 310,000, simu, king’amuzi na kikoi.
“Tukio la pili, lilikuwa ni Julai 4 mwaka huu saa 8: usiku, ambapo mama alichomewa nyumba eneo la Nyakato National ambayo ilikuwa inakaliwa na watu saba na wawili walipoteza maisha, ambao ni bibi mzaa mama, Yuritha Simon (87) na binti yake Monica Simon (30),” alisema.
Aliwataja walionusurika kifo katika tukio hilo la moto kuwa ni mama yake ambaye sasa ni marehemu, Vailet John ( 22), Thereza Simon (26), Annastazia Makoye (4), na mtoto mchanga Ndaki Makoye.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Valentino Mlowola, amethibitisha kupokea taarifa za tukio hilo na kwamba wanachunguza chanzo cha mauaji hayo.
Chanzo:Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mwanza Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa