Tone

Tone
Home » » ‘WANAWAKE ACHENI KUIKUMBATIA CCM’

‘WANAWAKE ACHENI KUIKUMBATIA CCM’

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Mwenyekiti ACT Mwanza, Pendo OjijoMWENYEKITI wa Chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT-Tanzania), Mkoa wa Mwanza, Pendo Ojijo, amewataka wanawake nchini kuachana na dhana ya kukikumbatia Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika masuala mbalimbali kwani kipo mstari wa mbele katika kuliteketeza Taifa la Tanzania.
Alisema wanawake ni jeshi kubwa lisilojitambua na kwamba, wakiamua kutumia nguvu walizonazo wanaweza kufanya mabadiliko makubwa ya kiuchumi na kisiasa ndani ya nchi.
Ojijo, alitoa kauli hiyo juzi katika mikutano ya hadhara iliyofanyika kata ya Nyambiti Wilaya ya Kwimba na Magu Mjini mkoani Mwanza.
Alisema licha ya wanawake kuwa waathirika wakubwa wa kushindwa kuwahjibika kwa serikali iliyopo madarakani, pia ndiyo wamekuwa wakikiunga mkono Chama Cha Mapinduzi kwa matumaini ya kupewa kanga na fulana siku ya uchaguzi.
“Wanawake tumekuwa wahanga wakubwa kutokana na serikali ya CCM kushindwa kutekeleza wajibu wake, tunafurahia kanga na kofia tunazoletewa siku ya uchaguzi na kukubali kuteseka kwa muda wa miaka minne baada ya kuwaweka madarakani watu wasiojali matumizi bora ya rasilimali za nchi,” alisema Ojijo.
Alisema viongozi waliyopo madarakani kwa sasa, wamekosa utu, uzalendo na hata moyo wa kuijali Tanzania, hali inayowafanya wajilimbikizie mali tofauti na misingi iliyoachwa na hayati baba wa Taifa, Mwalimu Julius
Nyerere.
 Chanzo;Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mwanza Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa