Tone

Tone
Home » » NGEREJA:TUTAONDOA KERO YA MAJI SENGEREMA

NGEREJA:TUTAONDOA KERO YA MAJI SENGEREMA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
 
MBUNGE wa Sengerema, William Ngeleja (CCM), ameishukuru Wizara ya Maji kwa kutenga zaidi ya sh. bilioni 29 kutekeleza miradi ya maji jimboni kwake.
Akizungumza na Tanzania Daima Jumapili jana, Ngeleja alisema hivi karibuni alifanya ziara jimboni kwake na kuona hatua mbalimbali za utekelezaji wa miradi hiyo.
Alisema ziara hiyo ililenga kukagua miradi ya maendeleo na utekelezaji wa ilani ya CCM ambapo waliohudhuria mikutano hiyo walionyesha kuridhishwa na utatuzi wa kero ya maji.
Ngeleja pia aliitaja miradi iliyotengewa fedha na inayoendelea kutekelezwa kupitia bajeti za miaka ya 2013/14 na 2014/15 ambayo ni Nyasigu-Lubungo- Ngoma ‘A’ (sh. bilioni 1. 6), Kasomeko- Chamabanda (sh. milioni 499.2), Chamabanda- Nyantakubwa (sh. milion 713.2), Nyantakubwa – Kasungamile (sh milion 250.5).
Mingine ni Katunguru-Nyamtelela (sh milioni 794.7), Nyamtelela-Nyamililo (sh. milioni 30), Buyagu-Kalangalala-Bitoto (sh bilioni 1.3), Busisi/Kahumulo- Nyampande (sh. milion 408), Chifunfu (sh. milioni 400), Kamanga-Nyamatongo (sh. milioni 405), na Nyamazugo -Sengerema mjini (sh. bilioni 23).
Ngeleja, alisema miradi hiyo itagharimu zaidi ya sh. bilioni 29 ambapo serikali itagharimia asilimia 100 isipokuwa mradi wa Nyamazugo- Sengerema mjini ambao umefadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AFDB) kupitia Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
“Kinachofurahisha zaidi ni kwamba miradi yote hii niliyoitaja hapa chanzo chake ni ziwa Victoria, kimsingi ni lazima tutoe pongezi kwa serikali inapotatua kero za wananchi,” alisema.
Chanzo:Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mwanza Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa